Waziri Mkuu Mpya wa Somalia atangaza baraza jipya la mawaziri 26
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i26676-waziri_mkuu_mpya_wa_somalia_atangaza_baraza_jipya_la_mawaziri_26
Waziri Mkuu Mpya wa Somalia leo ametangaza baraza lake la mawaziri 26 na kumteua waziri wa zamani wa mambo ya nje kuwa Waziri wa Fedha huku akimteuwa pia mwandishi wa habari wa BBC kuwa mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 21, 2017 10:48 UTC
  • Waziri Mkuu Mpya wa Somalia atangaza baraza jipya la mawaziri 26

Waziri Mkuu Mpya wa Somalia leo ametangaza baraza lake la mawaziri 26 na kumteua waziri wa zamani wa mambo ya nje kuwa Waziri wa Fedha huku akimteuwa pia mwandishi wa habari wa BBC kuwa mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa nchi hiyo.

Hassan Ali Khaire ambaye mwezi uliopita aliteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia, amesoma orodha ya majina ya baraza lake la mawaziri mbele ya waandishi wa habari. Rais Mohamed Abdullahi Mohamed  wa Somalia aliapishwa mwezi uliopita baada ya kumshinda Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud, ambaye uongozi wake ulikuwa ukikabiliwa na ukosoaji kutoka ndani na nje ya Somalia kwa masuala ya ufisadi.

Waziri Mkuu wa Somalia leo amemteuwa Abdirahman Duale Beyle kuwa Waziri wa Fedha na Yusuf Garaad Omar kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Profesa Abdirahman Duale Beyle ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha wa Somalia 

Beyle ambaye kitaaluma ni mchumi alikuwa akifanya kazi katika Benki ya Maendeleo ya Afrika, alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia kuanzia mwaka 2014 hadi 2015. Kwa upande wake, Yusuf Garaad Omar ambaye ana uraia wa nchi mbili za Somalia na Uingereza alikuwa mkuu wa kitengo cha matangazo ya lugha ya Kisomali katika Shirika la Utangazaji la BBC.