Mahakama ya Niger yawaachia huru watuhumiwa 15 wa jaribio la mapinduzi
Mahakama ya Niger imewaachia huru watu 15 waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za kupanga jaribio la mapinduzi dhidi ya Rais Mahamadou Issoufou wa nchi hiyo.
Watuhumiwa hao 15 waliachiwa huru jana ingawa wenzao 9 akiweno anayedaiwa kuwa kinara wa jaribio hilo, Jenerali Salou Souleymane, wangali wanashikiliwa na vyombo vya usalama.
Watuhumia hao walikamatwa Disemba 2015 baada ya serikali ya Niger kudai kuwa, imezima jaribio la mapinduzi ya kijeshi la kutaka kuchukua madaraka ya nchi kwa kutumia mabavu katika nchi hiyo ambayo ni mzalishaji mkubwa wa madini ya urani huko magharibi mwa Afrika.
Wakili wa watuhumiwa hao, Ali Kadri amesema kuwa tangu awali hakukuwepo ushahidi wa kuwahusisha na jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali ya Rais Mahamadou Issoufou.
Issoufou alichaguliwa tena kuwa Rais wa Niger katika uchaguzi uliofanyika mwezi Februari mwaka jana na kususiwa na kambi ya upinzani.