Zaidi ya watu 100 wauawa na kujeruhiwa nchini Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i29080-zaidi_ya_watu_100_wauawa_na_kujeruhiwa_nchini_somalia
Mtandao wa habari wa al Yaum al Saabi' wa nchini Misri umeripoti habari ya kuuawa na kujeruhiwa zaidi ya watu mia moja katika mapigano nchini Somalia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 14, 2017 08:20 UTC
  • Zaidi ya watu 100 wauawa na kujeruhiwa nchini Somalia

Mtandao wa habari wa al Yaum al Saabi' wa nchini Misri umeripoti habari ya kuuawa na kujeruhiwa zaidi ya watu mia moja katika mapigano nchini Somalia.

Mtandao huo umemnukuu Muhammad Ali, mkuu wa mkoa wa Jaldadu wa katikati mwa Somalia akisema kuwa, mapigano ya silaha yaliyotokea kwenye mkoa huo yamepelekea watu wasiopungua 6 kuuawa na wengine 99 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mapigano hayo yametokea kwa lengo la kudhibititi maeneo ya malisho na ya kilimo.

Somalia inahitajia misaada mingi ya dharura kutokana na kukumbwa na majanga mengi yakiwemo ya ukame, mashambulizi ya genge la kigaidi la al Shabab, uchache wa mvua na maradhi, mambo ambayo yamewaongezeka umaskini na njaa wananchi wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia katika mkutano wa kimataifa wa amani na usalama wa Somalia mjini London Uingereza 

 

Siku chache ziliopita pia, Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia aliiomba jamii ya kimataifa iisaidie nchi yake katika kupambana na ugaidi, ufisadi na umaskini wa kuchupa mipaka; mambo ambayo alisema ni adui mkuu wa nchi hiyo.

Rais Mohamed Abdullahi Mohamed alisema hayo katika mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia uliofanyika mjini London Uingereza kwa shabaha ya kurejesha amani na utulivu nchini humo.

Alisema, nchi yake inahitajia msaada wa kimataifa katika jitihada zake za kuwaletea ustawi wananchi wa nchi hiyo. Ikumbukwe kuwa Somalia ni moja ya nchi maskini zaidi na moja ya nchi zenye ukosefu mkubwa zaidi wa amani duniani.