UN yalaani kudharauliwa mauaji ya Waislamu wa CAR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i29344-un_yalaani_kudharauliwa_mauaji_ya_waislamu_wa_car
Umoja wa Mataifa umelaani kitendo cha vyombo vya habari duniani cha kudharau kuakisi habari yza mashambulizi na mauaji ya makumi ya Waislamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 20, 2017 08:15 UTC
  • UN yalaani kudharauliwa mauaji ya Waislamu wa CAR

Umoja wa Mataifa umelaani kitendo cha vyombo vya habari duniani cha kudharau kuakisi habari yza mashambulizi na mauaji ya makumi ya Waislamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, karibu Waislamu 30 wameuawa katika mji wa Bangassou kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na mashambulizi ya magenge yenye silaha, lakini vyombo vya habari duniani vimenyamaza kimya kana kwamba hakuna mauaji yoyote yaliyotokea.

Hadi hivi sasa maelfu ya raia Waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wameshauawa na kujeruhiwa na mamia ya maelfu ya wengine kukimbia makazi yao tangu nchi hiyo ilipokumbwa na machafuko ya kikaumu na kidini. Hata hivyo vyombo vya habari duniani vinapuuza kuakisi ukatili wanaofanyiwa Waislamu hao.

Magaidi wa Anti Balaka wanaofanya mauaji dhidi ya Waislamu Jamhuri ya Afrika ya Kati

 

Kwa mujibu wa maafisa wa Umoja wa Mataifa, mapigano ya hivi karibuni huko Jamhuri ya Afrika ya Kati yamefika pia kwenye kituo cha umoja huo na kushambuliwa na magenge yenye silaha.

Inadaiwa kuwa asilimia kubwa ya wakazi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ni Wakristo. Nchi hiyo iliingia kwenye machafuko mwaka 2013 baada ya kupinduliwa serikali ya nchi hiyo. Raia wengi wa nchi hiyo wamekuwa wakimbizi ndani na nje ya Jamhuri ya Afrika ya Kati huku wahanga wakuu wa machafuko hayo wakiwa ni raia Waislamu, mali na maeneo yao.