Wakimbizi wa Kiislamu Afrika ya Kati wana hali mbaya ya kibinaadamu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i30748-wakimbizi_wa_kiislamu_afrika_ya_kati_wana_hali_mbaya_ya_kibinaadamu
Habari kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati zinaarifu kwamba, jumla ya wakimbizi 1500 wa Kiislamu waliolazimika kuyahama makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo, wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinaadamu eneo la Bangassou nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 20, 2017 22:14 UTC
  • Wakimbizi wa Kiislamu Afrika ya Kati wana hali mbaya ya kibinaadamu

Habari kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati zinaarifu kwamba, jumla ya wakimbizi 1500 wa Kiislamu waliolazimika kuyahama makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo, wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinaadamu eneo la Bangassou nchini humo.

Waislamu hao waliyahama makazi yao kutokana na mapigano ya hivi karibuni baina ya waasi wa Seleka na Anti Balaka ambapo mamia ya watu waliuawa na maelfu ya wengine kuwa wakimbizi. Inaelezwa kuwa, awali mamia ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Kikristo la Anti-Balaka, walivamia msikiti wa mji huo wa Bangassou na wakamuua kwa namna ya kutisha imamu wa msikiti huo, kitendo ambacho kiliwatia wasi wasi Waislamu wanaoishi jirani na msikiti na kukimbilia katika kanisa moja mjini hapo ili kunusuru maisha yao.

Hali mbaya na masaibu yanayowakabili Waislamu wa CAR

Viongozi wa Kanisa Katoliki katika mji huo wametangaza kuwa, Waislamu hao ambao wanazingirwa na wapiganaji wa Kikristo katika kanisa hilo, wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinaadamu kutokana na kukosa huduma za kibinaadamu hususan chakula na mahitaji mengine ya msingi. Wakati huo huo, ujumbe wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, umetangaza kuwa, Waislamu hao wameshindwa kutoka ndani ya kanisa hilo kutokana na waasi hao wa Kikristo kuendesha doria kando na kanisa hilo kwa lengo la kutaka kuwaua.

Magaidi wa Kikristo wa Anti-Balaka wanaotekeleza mauaji dhidi ya Waislamu nchini humo

Habari zinasema kuwa, mashambulizi la magaidi hao wa Kikristo wa Anti-Balaka katika makazi ya Waislamu wa mji wa Bangassou yalikuwa ya kushtukiza na yaliyoratibiwa kwa ushirikiano wa baadhi ya askari wa serikali ya nchi hiyo.