Ripoti ya UN: Sudan Kusini haina tena baa la njaa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i30790-ripoti_ya_un_sudan_kusini_haina_tena_baa_la_njaa
Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu usalama wa chakula iliyotolewa Jumatano wiki hii imeeleza kuwa Sudan Kusini haiko tena katika kipengee cha nchi zilizoathiriwa na baa la njaa, japokuwa watu 45,000 katika mikoa ya Jonglei na Unity nchini humo wanatarajiwa kuendelea kukabiliwa na hali ngumu na kwamba hali ya mambo hata hivyo bado ni mbaya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 21, 2017 23:50 UTC
  • Ripoti ya UN: Sudan Kusini haina tena baa la njaa

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu usalama wa chakula iliyotolewa Jumatano wiki hii imeeleza kuwa Sudan Kusini haiko tena katika kipengee cha nchi zilizoathiriwa na baa la njaa, japokuwa watu 45,000 katika mikoa ya Jonglei na Unity nchini humo wanatarajiwa kuendelea kukabiliwa na hali ngumu na kwamba hali ya mambo hata hivyo bado ni mbaya.

Watu wanaokadiriwa milioni sita, ambayo ni nusu ya jamii ya nchi hiyo,  wanatazamiwa kuathiriwa vibaya na uhaba wa chakula mwezi huu na ule ujao; kiwango ambacho kimeongezeka kulinganisha na kile cha mwezi Mei ambapo raia wa Sudan Kusini milioni 5.5 waliathiriwa na uhaba wa chakula. 

Watoto wa Sudan Kusini wakiwa katika safu ya mgawo wa chakula kufuatia baa la njaa lililoiathiri nchi yao

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa kuhusu usalama wa chakula imetolewa kwa kutegemea utafiti uliofanywa na jopo kazi lililozishirikisha serikali ya Juba na maafisa wa Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, hakuna tena baa la njaa katika kaunti za kaskazini mwa Sudan Kusini ambako janga hilo lilitangazwa mwezi Februari mwaka huu.