Wapiganaji 13 wa kundi la Mai-Mai wauawa na jeshi la DRC
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i30872-wapiganaji_13_wa_kundi_la_mai_mai_wauawa_na_jeshi_la_drc
Wapiganaji kadhaa wa kundi la wanamgambo wa Mai-Mai katika Jamhutri ya Kidemokrasia ya Congo wameuawa kufuatia operesheni ya jeshi la nchi hiyo katika mji wa Bunia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 23, 2017 09:51 UTC
  • Wapiganaji 13 wa kundi la Mai-Mai wauawa na jeshi la DRC

Wapiganaji kadhaa wa kundi la wanamgambo wa Mai-Mai katika Jamhutri ya Kidemokrasia ya Congo wameuawa kufuatia operesheni ya jeshi la nchi hiyo katika mji wa Bunia.

Msemaji wa operesheni ya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema kuwa, wapiganaji 13 wa Mai-Mai wameuawa kufuatia shambulio la jeshi katika mji wa Bunia ulioko katika mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Jules Ngongo amewaambia waandishi wa habari kwamba, mbali na wanamgambo 13 wa kundi la Mai-Mai kuuawa katika shambulio hilo, jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limewatia mbaroni wanachama 13 wa kundi hilo.

Msemaji huyo wa jeshi la Congo DR sambamba na kuashiria kuondoka waasi wa Mai-Mai katika mji wa Bunia amesema kuwa, jeshi la serikali ya nchi hiyo limekuwa likisaidiwa na kikosi cha kusimamia amani cha Umoja wa Mataifa katika kuwasaka na kuwafuatia wanamgambo hao ambao wameharatisha usalama katika maeneo hayo.

waasi wa Mai-Mai

Wakati huo huo, wajumbe 47 wa Mataifa yanayounda Baraza la Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa wameafikiana na serikali ya Kinshasa juu ya kutounda tume ya kimataifa kwa ajili ya  kuchunguza mauaji ya Kasai na badala yake serikali Kinshasa itawezeshwa kiufundi kwa ajili ya kuendesha uchunguzi huo yenyewe.

Serikali ya Kinshasa imekua ikilaumiwa kufuatia mauaji yaliyotokea katika mkoa wa Kasai, wakati ambapo serikali hiyo imeendelea kuyalaumu mashirika yasiyo ya kiserikali na baadhi ya mataifa ya Magharibi kwa kuchochea vurugu katika nchi hiyo.