Umoja wa Mataifa kutuma wataalamu wa Kimataifa, Kasai, DRC
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i30896-umoja_wa_mataifa_kutuma_wataalamu_wa_kimataifa_kasai_drc
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio la kutuma wataalamu wa kimataifa katika eneo la Kasai la katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 24, 2017 02:39 UTC
  • Umoja wa Mataifa kutuma wataalamu wa Kimataifa, Kasai, DRC

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio la kutuma wataalamu wa kimataifa katika eneo la Kasai la katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa lilitoa azimio mjini Geneva Uswisi na kusema kuwa, umoja huo umeamua kutuma wataalamu wa kimataifa nchini Kongo kwa ajili ya kuchunguza mapigano na machafuko yaliyotokea katika eneo la Kasai.

Aidha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limemtaka Zeid Ra’ad Al Hussein, kamishna mkuu wa haki za binadamu wa umoja huo atoe ripoti ya uchunguzi huo katika kikao cha kawaida cha 37 cha baraza hilo.

Makaburi ya umati katika eneo la Kasai, DRC

 

Makanisha ya Kikatoliki yamesema kuwa, zaidi ya watu elfu tatu wameshauawa hadi hivi sasa tangu yalipozuka mapigano katika eneo la Kasai mwaka jana.

Umoja wa Mataifa aidha umesema kuwa, watu milioni 1.3 wameyakimbia makazi yao katika eneo hilo la katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na machafuko hayo. Watu 30 elfu wamekimbilia katika nchi jirani ya Angola.