Uongozi mbaya, sababu ya mgogoro wa wawakimbizi barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i30898-uongozi_mbaya_sababu_ya_mgogoro_wa_wawakimbizi_barani_afrika
Viongozi wa nchi za Afrika wamesema kuwa, uongozi mbaya wa watawala wa bara hilo ndio unaoitishwa Afrika mgogoro wa wakimbizi.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jun 24, 2017 02:43 UTC
  • Uongozi mbaya, sababu ya mgogoro wa wawakimbizi barani Afrika

Viongozi wa nchi za Afrika wamesema kuwa, uongozi mbaya wa watawala wa bara hilo ndio unaoitishwa Afrika mgogoro wa wakimbizi.

Wakuu wa nchi za Afrika zilizovamiwa na wimbi la wakimbizi walisema hayo jana mjini Kampala, Uganda na kuongeza kuwa, utawala mbaya, uongozi usiofaa na dhaifu ndiyo sababu kuu ya kuvamiwa nchi hizo na wimbi kubwa la wakimbizi kutoka maeneo mengine.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema hayo katika "kikao cha mshikamano" na kuongeza kuwa, taasubu za kikabila na kukosekana wapinzani wa kuaminika ni katika mambo yanayozusha mapigano ya umwagaji wa damu katika baadhi ya nchi za Kiafrika ambayo yanawalazimisha wakazi wa nchi hizo kuyakimbia makazi yao.

Wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Uganda

 

Ukitoa Uturuki na Pakistan, Uganda ni nchi ya tatu yenye wakimbizi wengine duniani na ni ya kwanza barani Afrika. Hivi sasa kuna wakimbizi karibu milioni moja wa Sudan Kusini pekee nchini Uganda.

Kwa upande wake, António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye alishiriki katika "Kikao cha Mshikamano" cha mjini Kampala, Uganda amesema, kuna udharura wa kuongezwa juhudi za kukomeshwa migogoro barani Afrika ukiwemo wa Sudan Kusini.