Maeneo yanayozalisha mafuta Tunisia yatangazwa kuwa ya kijeshi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31110-maeneo_yanayozalisha_mafuta_tunisia_yatangazwa_kuwa_ya_kijeshi
Baraza la Usalama wa Taifa la Tunisia limeyatangaza maeneo yanayozalisha mafuta na maliasili nchini humo kuwa ni maeneo ya kijeshi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 29, 2017 03:21 UTC
  • Maeneo yanayozalisha mafuta Tunisia yatangazwa kuwa ya kijeshi

Baraza la Usalama wa Taifa la Tunisia limeyatangaza maeneo yanayozalisha mafuta na maliasili nchini humo kuwa ni maeneo ya kijeshi.

Tangazo hilo la kuyaarifisha maeneo hayo kuwa ni ya kijeshi lilipasishwa katika kikao kilichoongozwa na Rais Beji Caid al Sebsi wa Tunisia kilichochunguza hali ya usalama na ya ndani ya nchi; na kutupia jicho pia hali ya kieneo na kimataifa.

Rais Beji Caid al Sebsi wa Tunisia 

 Kikao hicho kilichoongozwa na Rais wa Tunisia kimetilia mkazo suala la kuzidisha ushirikiano kati ya nchi hiyo na nchi zinazoendesha mapambano dhidi ya ugaidi ili kutokomeza na kuzuia kupenya ugaidi katika eneo.

Kabla ya kikao hicho, Wizara ya Ulinzi ya Tunisia ilitahadhrisha kuhusu maafa yatakayosabishwa na shambulio lolote katika vituo na taasisi za mafuta za nchi hiyo kufuatia shambulio lililotekelezwa na wapinzani wa serikali. Wizara hiyo imesisitiza kuwa hali ya usalana na utulivu inashuhudiwa katika taasisi za mafuta za nchi hiyo kufuatia kuwepo vikosi vya jeshi na askari usalama na kwamba utendaji kazi katika taasisi hizo utarejea katika hali ya kawaida.