Qatar yasusia bidhaa za nchi nne za Kiarabu
(last modified Sat, 01 Jul 2017 07:19:34 GMT )
Jul 01, 2017 07:19 UTC
  • Qatar yasusia bidhaa za nchi nne za Kiarabu

Wananchi wa Qatar wamesusia bidhaa za nchi nne za Saudi Arabia, Imarati, Bahrain na Misri baada ya nchi hizo kuendeleza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi yao.

Bidhaa zinazozalishwa na makampuni kadhaa ya Saudia na Imarati hususan kampuni inayotengeneza bidhaa za maziwa ya al Marai zimeanza kususiwa na wananchi wa Qatar. Kampuni ya al Marai ndiyo kampuni kubwa inayotengeneza bidhaa zitokanazo na maziwa katika eneo la Mashariki ya Kati na soko kubwa huko Qatar kwa kuuza nchini humo asilimilia 80 ya bidhaa zake za chakula.

Kampuni ya al Marai ya Saudia iliyosusiwa na wananchi wa Qatar

Tahfifu makhsusi iliyotolewa kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa nchini Saudi Arabia na Imarati pia imeshindwa kuwavutia na kuwashawishi raia wa Qatar ili wazinunue katika maduka makubwa ya nchi hiyo. 

Saudia na nchi waitifaki wake wanaituhumu Qatar kuwa inayaunga mkono makundi yenye misimamo mikali na zimeamua kukata uhusiano wao na nchi hiyo. Qatar imekanusha tuhuma hizo na kuitaja hatua ya nchi hizo kuwa ni mzingiro dhidi ya Qatar. Saudi Arabia, Imarati na Bahrain imesimamisha  njia zote za usafiri wa  baharini, nchi kavu na anga kati yao na Qatar. 

Tags