Jeshi la Kongo lakomboa baadhi ya maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31332-jeshi_la_kongo_lakomboa_baadhi_ya_maeneo_ya_mashariki_mwa_nchi_hiyo
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeyakomboa baadhi ya maeneo ya jimbo la Fizi mkoani Kivu ya Kusini mashariki mwa nchi hiyo kutoka mikononi mwa waasi wa Mai-Mai.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 04, 2017 10:41 UTC
  • Jeshi la Kongo lakomboa baadhi ya maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeyakomboa baadhi ya maeneo ya jimbo la Fizi mkoani Kivu ya Kusini mashariki mwa nchi hiyo kutoka mikononi mwa waasi wa Mai-Mai.

Safari Gustave Bwange, kamanda wa oparesheni ya "Sokola 2" na 3" ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mkoa wa Kivu ya Kusini amesema kuwa, jeshi la nchi hiyo limewafurusha waasi wa Mai-Mai katika maeneo ya Nyange na Ngalula katika eneo la Fizi.

Waasi wa Mai-Mai wanaopigana na jeshi la serikali ya Kongo DR 

Gustave Bwange ameongeza kuwa, wakazi wa maeneo hayo ya mashariki mwa Kongo wameyakimbia makazi yao kufuatia mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi. Kamanda wa jeshi la Kongo amesisitiza kuwa, wafanyabishara wa miji ya kandokando na mkoa wa Kivu ya Kusini wanakabiliwa na hali ngumu katika shughuli zao kutokana na  mapigano hayo.

Waasi wa Mai-Mai Jumamosi iliyopita waliyavamia na kuyakalia baadhi ya maeneo ya jimbo la Fizi baada ya kukabiliana na wanajeshi wa serikali.