Misri kuchunguza mauaji ya raia wake nchini Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31542-misri_kuchunguza_mauaji_ya_raia_wake_nchini_libya
Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imetangaza kuwa, itafanya uchunguzi kuhusu maiti za raia 19 wa nchi hiyo zilizopatikana katika eneo la jangwani kaskazini mashariki mwa Libya.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Jul 09, 2017 09:33 UTC
  • Misri kuchunguza mauaji ya raia wake nchini Libya

Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imetangaza kuwa, itafanya uchunguzi kuhusu maiti za raia 19 wa nchi hiyo zilizopatikana katika eneo la jangwani kaskazini mashariki mwa Libya.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, Ahmad Abu Zaid amesema kuwa, Cairo imepata taarifa kupitia taasisi za Hilali Nyekundu ya Libya kwamba, maiti za raia 19 wa nchi hiyo zimepatikana katika eneo la jangwani huko Tobruk na Ajdabiya kaskazini mwa Libya. 

Abu Zaid ameongeza kuwa, hadi sasa maiti 7 kati yao 19 zilizopatikana zimetambulika na kurejeshwa nchini Misri. 

Afisa huyo wa serikali ya Misri amesema kuwa, inaonekana Wamisri hao waliokuwa wahajiri haramu, waliuawa na wafanya magendo ya binadamu.

Libya ilitumbukia katika machafuko ya ndani na ukosefu wa serikali kuu baada ya majeshi ya Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi (NATO) kushambulia nchi hiyo na kuwawezesha wanamapinduzi wa nchi hiyo kumuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.