Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakaribisha mazungumzo ya Libya
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekaribisha kufanyika mazungumzo ya kisiasa kati ya mirengo ya upinzani huko Libya.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekaribisha kikao cha hivi karibuni kati ya mirengo ya upinzani ya Libya kilichofanyika kwa lengo la kusogeza mbele mazungumzo ya kisiasa nchini humo. Baraza la Usalama pia limesema linatiwa wasiwasi na kuendelea vitisho vya kigaidi nchini Libya.
Taarifa iliyotolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa mazungumzo ya kisiasa kati ya mirengo ya upinzani huko Libya yanaonyesha kuwepo azma thabiti kati ya mirengo hiyo kwa minajili ya kufikia muafaka wa kisiasa.
Wakati huo huo Ban Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia ameunga mkono kuwepo msimamo wa pamoja kati ya mirengo ya Libya kwa lengo la kurejesha amani na uthabiti nchini humo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa nchi wanachama wa baraza hilo linaiomba serikali ya kitaifa ya Libya kutekeleza hatua za lazima ili kurejesha uthabiti nchini humo.