Machafuko yaendelea katika mpaka wa Niger na Mali
(last modified Sat, 22 Jul 2017 16:35:20 GMT )
Jul 22, 2017 16:35 UTC
  • Machafuko yaendelea katika mpaka wa Niger na Mali

Machafuko na mapigano makali yameendelea kushuhudiwa katika eneo la mpaka wa Niger na Mali licha ya kutangazwa ripoti ya mafanikio makubwa ya Operesheni ya Barkhane katika eneo hilo.

Jeshi la Ufaransa likishirikiana na majeshi ya nchi za Niger na Mali limeanzisha mashambulizi makali katika mpaka wa nchi hizo mbili katika kile kilichopewa jina la Operesheni ya Barkhane lakini ripoti zinasema machafuko na hali ya ukosefu wa amani vingali vinatawala eneo hilo licha ya kutolewa ripoti za kufanikiwa opesheni hiyo.

Zaidi ya askari elfu moja wa Ufaransa na magari 200 ya kijeshi walipelekwa katika eneo la mpaka wa Mali na Niger tarehe 6 mwezi huu wa Julai kukabiliana na kundi la waasi la Soudoubaba. Askari 8 wa Mali wamekamatwa mateka na kuuawa na waasi hao. 

Askari wa Ufaransa katika mpaka wa Mali na Niger

Jeshi la Mali sasa linachunguza uwezekano wa kuanzisha doria na kuchukua hatua kali za kiusalama katika eneo hilo ili kukabiliana na machafuko hayo. 

Serikali ya Mali hadi sasa haijafanikiwa kutekeleza makubaliano ya amani ya mwaka 2015 na makundi ya waasi na hadi sasa maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo yangali yanasumbuliwa na machafuko na mashambulizi ya mara kwa mara.  

Tags