Viwiliwili vya wahajiri 16 vyapatikani jangwani mashariki mwa Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i33973-viwiliwili_vya_wahajiri_16_vyapatikani_jangwani_mashariki_mwa_libya
Vikosi vya usalama nchini Libya vimetangaza habari ya kupatikana miili 16 ya wahajiri katika eneo la jangwani, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Misri.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 06, 2017 02:40 UTC
  • Viwiliwili vya wahajiri 16 vyapatikani jangwani mashariki mwa Libya

Vikosi vya usalama nchini Libya vimetangaza habari ya kupatikana miili 16 ya wahajiri katika eneo la jangwani, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Misri.

Ahmed al-Mismari, msemaji wa Jeshi la Taifa la Libya mashariki mwa nchi amesema maiti hizo zimepatikana yapata kilomita 310 kusini magharibi mwa mji wa bandari wa Tobruk.

Afisa huyo wa Jeshi la Libya mashariki mwa nchi amesema kwa sasa wanafanya shughuli za kubaini utambulisho wa miili hiyo sanjari na kutafuta miili zaidi katika jangwa hilo.

Haya yanajiri siku chache baada ya kikosi cha gadi ya pwani ya Libya kiwaokoa wahajiri zaidi ya 300 katika maji ya magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.

Mmoja wa wahajiri waliotelekezwa jangwa la Sahara

 

Mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, wahamiajia 50 wa Kiafrika waliripotiwa kufariki dunia katika jangwa la Sahara huko kaskazini mwa Niger baada ya kutelekezwa na madereva wao.

Aghalabu ya wahajiri hao haramu ambao kutokana na sababu za kiuchumi huamua kuziacha nchi zao kwa tamaa ya kwenda kutafuta kazi na maisha mazuri barani Ulaya, hutokea katika nchi za Nigeria, Eritrea, Niger Somalia, Sudan, Gambia, Senegal, Mali, Morocco na Tunisia.