Fayez al Sarraj aitolea wito Algeria kushiriki katika mazungumzo ya kitaifa ya Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i37771
Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya ameitaka Algeria ishiriki pakubwa katika kusogeza mbele mazungumzo ya kusaka amani ya nchi yake.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 18, 2017 14:30 UTC
  •  Fayez al Sarraj aitolea wito Algeria kushiriki katika mazungumzo ya kitaifa ya Libya

Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya ameitaka Algeria ishiriki pakubwa katika kusogeza mbele mazungumzo ya kusaka amani ya nchi yake.

Akizungumza jana mjini Algiers akiwa ziarani Algeria, Fayez al Sarraj amewatolea wito viongozi wa nchi hiyo kuishinikiza zaidi Misri ili serikali ya Cairo isitishe uungaji mkono wake kwa Meja Jenerali Khalifa Haftar kamanda wa jeshi la taifa la Libya.  

Al Sarraj amesema kuwa amebainisha wazi katika mazungumzo yake na viongozi wa Algeria kwamba, kuendelea kuungwa mkono Khalifa Haftar kukiwemo kumuunga mkono katika mapambano dhidi ya ugaidi;  kutafelisha jitihada za kimataifa za kutekeleza mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuendesha uchaguzi mkuu huko Libya ukiwemo uchaguzi wa rais mnamo tarehe 9 mwezi ujao. 

Meja Jenerali Khalifa Haftar ambaye ni hasimu wa Waziri Mkuu wa Libya, Fayez al Sarraj 
 

Meja Jenerali Khalifa Haftar ambaye ni kamanda wa jeshi la taifa la Libya jana aliutaja Umoja wa Mataifa na serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al Sarraj kuwa sababu ya kuvunjika mazungumzo na kueleza kuwa, itibari ya makubaliano yote yaliyofikiwa kuanzia Geneva hadi Sakhirat yamefikia tamati na kwamba hatosalimu amri mbele ya vitisho. Mwaka 2011 Libya ilikumbwa na mgogoro wa kisiasa na kutumbukia katika hali ya mchafukoge na mapigano kati ya makundi ya kikabila ya nchi hiyo kufuatia uingiliaji kijeshi wa Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi. Nchi hiyo imekuwa ikiongozwa na mamlaka mbili moja ikiwa ni jeshi la taifa linaloongozwa na Kamanda Haftar huko Tobruk na serikali ya Fayez al Sarraj yenye makao yake huko Tripoli.