Mwendesha mashtaka wa Misri ataka kufuatiliwa vyombo vya habari nchini humo
(last modified Wed, 28 Feb 2018 16:31:19 GMT )
Feb 28, 2018 16:31 UTC
  • Mwendesha mashtaka wa Misri ataka kufuatiliwa vyombo vya habari nchini humo

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Misri ametaka kufuatiliwa kwa kina na kwa karibu shughuli za vyombo vya habari na kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi ya chombo chochote cha habari ambacho kinavuruga usalama na kuhatarisha maslahi ya taifa.

Ofisi ya Nabil Sadeq leo Jumatano imetoa taarifa ikiagiza wafanyakazi wake kufuatilia kwa karibu shughuli za vyombo vya habari. Taarifa hiyo imesema kuwa, hatua zinapaswa kuchukuliwa kukabiliana na kile kilichotajwa kuwa "jitihada za nguvu za kishetani" za kutaka kudhoofisha hali ya usalama na amani ya taifa kupitia kutangaza na kueneza taarifa za uwongo.

Istilahi hiyo ya "jitihada za nguvu za kishetani" iliyotumiwa katika taarifa ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Misri imekuwa ikitumiwa mara kwa mara na serikali ya Rais Abdel Fattah al Sisi kudhihirisha upinzani wake kwa wale wote waliokaribu na harakati ya Ikhwanul Muslimin ya nchini humo inayohesabiwa kuwa kundi kubwa zaidi la kisiasa lenye nguvu huko Misri na kongwe zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu ambalo limepigwa marufuku kuendesha shughuli zake tangu Abel Fattah al Sisi alipotwaa madaraka ya nchi mwaka 2014.

Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri 

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Misri imetoa taarifa hiyo ukiwa umesalia mwezi mmoja kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais nchini humo.

Tags