Mkuu wa Baraza Kuu la Serikali Libya anusurika jaribio la kumuua
Idara ya Habari ya Mkuu wa Baraza Kuu la Serikali ya Libya imetangaza kuwa, kiongozi huyo na ujumbe uliokuwa ukiandamana naye umenusurika jaribio la kuuawa huko magharibi mwa nchi hiyo.
Idara hiyo imetangaza kuwa, gazri la Abdulrahman Sewehli na wapambe wake limeshambuliwa kwa risasi wakati alipokiwa kitembelea miji miwili ya magharibi mwa Libya.
Taarifa hiyo imesema kuwa, askari wawili waliokuwa wakilinda msafara wa Abdulrahman Sewehli wamejeruhiwa na polisi wengine wanne wametekwa nyara.
Hii ni mara ya pili Mkuu wa Baraza Kuu la Serikali ya Libya kunusruka jaribio la kutaka kumuua.
tarehe 20 Februari Abdulrahman Sewehli na Waziri Mkuu wa serikali ya mwafaka wa kitaifa Faiz al Sarraj walinusurika jaribio kama hilo mjini Tripoli.
Umoja wa Mataifa umelaani shambulizi hilo lililolenga msafara wa Abdulrahman Sewehli na kutoa wito wa kukomeshwa machafuko kwa ajili ya kufikia mapatano kamili ya kisiasa nchini Libya.