UN yakemea kutekwa nyara Mwendesha Mashtaka wa Jeshi Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i41954-un_yakemea_kutekwa_nyara_mwendesha_mashtaka_wa_jeshi_libya
Kikosi cha Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa nchini Libya kimetoa wito wa kuchukuliwa hatua za dharura za kulinda usalama wa Mwendesha Mashtaka wa Jeshi nchini Libya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 21, 2018 00:35 UTC
  • UN yakemea kutekwa nyara Mwendesha Mashtaka wa Jeshi Libya

Kikosi cha Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa nchini Libya kimetoa wito wa kuchukuliwa hatua za dharura za kulinda usalama wa Mwendesha Mashtaka wa Jeshi nchini Libya.

Ofisi ya kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa imeeleza wasiwasi wake kuhusu kitendo cha kutekwa nyara Mwendesha Mashtaka wa Jeshi la Libya, Massoud Erhuma na kusema, ni pigo kubwa kwa utawala wa sheria na usalama wa Libya. 

Ripoti zinasema kuwa, watu wasiojulikana waliokuwa na silaha Alkhamisi iliyopita walimteka nyara Massoud Erhuma mbele ya nyumba yake mjini Tripoli na kwamba hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na kitendo hicho. 

Libya imetumbukia katika machafuko ya ndani

Kamisheni ya Taifa ya Haki za Binadamu nchini Libya pia imeutaja utekaji nyara huo kuwa ni kuwavunjia heshima viongozi wa vyombo vya mahakama na imetoa wito wa kufanyika uchunguzi na kuwachukulia hatua wahusika. 

Libya ilitumbukia katika ghasia na machafuko makubwa ya ndani baada na kuondolewa madarakani na kuuawa dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi mwaka 2011.