Boko Haram wafanya shambulizi kaskazini mashariki mwa Nigeria watu 18 wauawa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i42540-boko_haram_wafanya_shambulizi_kaskazini_mashariki_mwa_nigeria_watu_18_wauawa
Duru za habari nchini Nigeria zimeripoti kwamba, kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram limefanya shambulizi katika mji wa Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
(last modified 2025-11-23T06:16:50+00:00 )
Apr 02, 2018 14:29 UTC
  • Boko Haram wafanya shambulizi kaskazini mashariki mwa Nigeria watu 18 wauawa

Duru za habari nchini Nigeria zimeripoti kwamba, kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram limefanya shambulizi katika mji wa Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Habari zinasema kuwa, shambulizi hilo limefanyika leo na kwamba kwa akali watu 18 wameuawa na wengine 84 kujeruhiwa. Kwa mara kadhaa jimbo la Borno limekuwa likikumbwa na mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa na magaidi hao wa Boko Haram. Genge hilo lilianzisha hujuma zake nchini Nigeria na katika nchi jirani na taifa hilo tangu mwaka 2009 ambapo hadi sasa zaidi ya watu 20 elfu wameshauawa na wengine milioni mbili na laki sita kuwa wakimbizi.

Jinai za kundi la Boko Haram dhidi ya raia wa kawaida Nigeria

Udhaifu wa nchi za eneo la Ziwa Chad katika kukabiliana na kundi hilo linalofuata aidolojia ya Uwahabi, unatajwa kuwa chanzo cha kuendelea mashambulizi hayo ya mara kwa mara.

Hivi karibuni Waziri wa Habari wa Nigeria alinukuliwa akisema kuwa, serikali ya nchi hiyo inafanya mazungumzo na kundi hilo la Boko Haram juu ya uwezekano wa kusitisha mapigano, lengo kuu likiwa ni kukomesha kikamilifu uadui na uhasama baina ya pande mbili. 

Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa serikali ya Abuja kutangaza kuwa inafanya mazungumzo na Boko Haram kuhusu usitishaji mapigano yaliyosababisha maelfu ya watu kuuawa nchini Nigeria.