Apr 07, 2018 15:56 UTC
  • Kulazimishwa kujiuzulu Jacob Zuma kumezusha mgogoro wa kisiasa Afrika Kusini

Kitendo cha kulazimishwa Jacob Zuma kujiuzulu urais kabla ya kumalizika muda wake huko Afrika Kusini si tu kimekiathiri chama tawala cha ANC, lakini pia kimezusha mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Mtandao wa habari wa Swissinfo umeripoti habari kuhusu matokeo mabaya ya kulazimishwa kujiuzulu urais Jacob Zuma huko Afrika Kusini kwa kuandika kuwa, kitendo cha kulazimishwa Zuma kujiuzulu kabla ya kumalizika kipindi chake cha urais kilichokuja baada ya wiki kadhaa za mgogoro, kimezusha mpasuko ndani ya chama tawala cha ANC na kimepelekea pia kuakhirishwa hotuba ya kila mwaka ya serikali katika bunge la nchi hiyo.

Naye Spika wa Bunge la Afrika Kusini Baleka Mbete amesema, amelazimika kuakhirisha hotuba ya serikali mbele ya bunge hilo kutokana na kuzuka mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Bunge la Afrika Kusini

 

Itakumbukwa kuwa kesi inayomkabili Jacob Zum imeakhirishwa hadi Juni 8 mwaka huu baada ya rais huyo wa zamani kupandishwa kizimbani katika Mahakama Kuu ya Durban akikabiliwa na tuhuma za ufisadi wa mali ya umma unaohusiana na kashfa ya silaha.

Kesi ya Zuma haikuchukua zaidi ya robo saa kabla ya kuakhirishwa hadi Juni nane mwaka huu baada ya mawaikili wake kusema kuwa wanahitaji muda zaidi wa kukusanya ushahidi wa kumtetea mteja wao. Taarifa zinasema kuwa, iwapo Jacob Zuma atapatikana na hatia anaweza kufungwa hadi miaka 15 jela, ingawa yeye mwenyewe amekuwa akisisitiza kuwa hana hatia na atalithibitisha hilo kwa kila mtu. 

Huko nyuma chama chake cha ANC kilisema kuwa hakitojihusisha na kesi hiyo kama chama, lakini wanachama wake wanaweza kufanya hivyo kwa sharti wasifanye kwa jina la chama.

Tags