Siyala: Uingiliaji wa nchi ajinabi; chanzo kikuu cha machafuko Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i43144-siyala_uingiliaji_wa_nchi_ajinabi_chanzo_kikuu_cha_machafuko_libya
Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya amekosoa uingiliaji wa nchi ajinabii kuwa sababu kuu inayosababisha hali ya machafuko na ukosefu wa amani nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 15, 2018 09:45 UTC
  • Siyala: Uingiliaji wa nchi ajinabi; chanzo kikuu cha machafuko Libya

Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya amekosoa uingiliaji wa nchi ajinabii kuwa sababu kuu inayosababisha hali ya machafuko na ukosefu wa amani nchini humo.

Mohammed al Tahir Siyala amesema kuwa rasimu ya kisheria kuhusu njia ya ufumbuzi wa kisiasa huko Libya imewasilishwa kulingana na taarifa ya Niger kuhusu hali ya usalama kusini mwa nchi hiyo. Siyala ameongeza kuwa hali ya usalama kusini mwa Libya inatisha kutokana na uingiliaji wa nchi ajinabi na kwa sababu hiyo tarehe tatu mwezi huu kulifanyika kikao kilichohudhuriwa na Niger, Chad na Sudan.

Hali ya kutisha ya usalama  kusini mwa Libya 

Ameongeza kuwa katikati ya mwezi Mei pia kutafanyika kikao kingine huko Chad na  mwishoni mwa mwezi Mei kutafanyika kikao kingine cha kundi la Kiarabu na Afrika katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya amebainisha kuwa kikao cha Niamey kimekuwa na mchango katika kupunguza oparesheni za magaidi huko Libya kwa sababu kikao hicho kilisisitiza kuzingatiwa pakubwa suala la usalama katika mipaka ya pamoja. Libya imekumbwa na hali ya mchafukoge tangu kupinduliwa madarakani dikteta wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mwaka 2011 kufuatia uingiliaji wa kijeshi wa Marekani nchini humo.