Uingiliaji wa kigeni, sababu kuu ya ukosefu wa amani nchini Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i43196-uingiliaji_wa_kigeni_sababu_kuu_ya_ukosefu_wa_amani_nchini_libya
Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Libya amekosoa uingiliaji wa madola ya kigeni na kusema kwamba, sababu kuu ya nchi hiyo kushuhudia ukosefu wa usalama na amani ni uingiliaji wa madola hayo katika masuala ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 16, 2018 22:48 UTC
  • Uingiliaji wa kigeni, sababu kuu ya ukosefu wa amani nchini Libya

Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Libya amekosoa uingiliaji wa madola ya kigeni na kusema kwamba, sababu kuu ya nchi hiyo kushuhudia ukosefu wa usalama na amani ni uingiliaji wa madola hayo katika masuala ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Mohamed Taher Siala ameashiria muswada wa katiba ya Libya ambao umejikita katika utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa nchi hiyo na kuonya kwamba, usalama kusini mwa nchi hiyo umo hatarini kutokana na uingiliaji wa madola ya kigeni. Kuendelea mgogoro nchini Libya na kutokuweko serikali kuu yenye nguvu kumeifanyya nchi hiyo iendelee kushuhudia ukosefu wa amani na usalama pamoja na harakati za makundi ya kigaidi.

Filihali kuna makundi ya kisiasa, wanamgambo na magaidi mbalimbali nchini Libya ambapo akthari ya makundi hayo yanaungwa mkono na madola ya kigeni kwa siri au kwa dhahiri. Mpasuko wa wazi unaoonekana ndani ya Libya ni kuungwa mkono na madola ya Magharibi na Umoja wa Mataifa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya nchi hiyo huku serikali inayoongozwa na jenearli mstaafu Khalifa Haftar yenye makao yake makuu masharikki mwa Libya ikiungwa mkono na Imarati, Misri na Saudi Arabia.

Mohamed Taher Siala, Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Libya

Timu ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni ilisema katika ripoti yake kwamba, Imarati ipo nchini Libya na imekuwa ikipanua uwepo wake bila ya mwafaka wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya nchi hiyo. Baadhi ya ripoti zinaonyesha kwamba, kuna baadhi ya makundi ya wabeba silaha ya Kiafrika kutoka Chad, Niger na Sudan Kusini ambayo yanafanya harakati zake nchini Libya. 

Hali hiyo imewafanya viongozi wa Libya na wataalamu wa masuala yya kisiasa kutahadharisha kuhusu hatari ya kugawanyika nchi hiyo.

Aqila Saleh, Spika wa Bunge la Libya amesema kuhusiana na jambo hilo kwamba, adui ajinabi anafanya njama za kuigawa Libya  hivyo basi haipasi kuwaruhusu wageni waicheze shere mamlaka ya kujitawala na ardhi yote ya nchi hiyo. Pengo na mgogoro wa kisiasa nchini Libya kwa muda sasa umekwamisha mwenendo wa kudhibiti na kulinda mamlaka ya ardhi ya nchi hiyo. Jambo hilo limeyafanya makundi mbalimbali ya kigaidi, wanamgambo na magenge ya magendo ya binadamu na madawa ya kulevya kuwa na harakati zao katikka maeneo mbalimbali yya nchi hiyo hususan kusini mwa nchi hiyo.

Machafuko ya Libya

Nafasi ya kijiografia ya Libya na uwepo wa vyanzo vya utajiri kama mafuta na gesi nchini Libya ni mambo ambayo yyameifanyya nchi hiyo itazamwe kwa jicho la tamaa sio na madola ya Magharibi tu bali hata baadhi ya  nchi za Kiarabu kama Imarati na Saudi Arabia. Madola hayo yamekuwa yakifanya kila yawezalo kuongeza satua na ushawishi wao nchini Libya kwa kuyaunga mkono makundi mbalimbali ya wanamgambo na hivyo kuzuia kupatikana umoja na uthabiti wa kisiasa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. 

Miftah Bou Khalil, meya wa mji wa Kufra ameashiria mpasuko na mgogoro wa kiusalama na kisiasa nchini Libya  na kusema kuwa, mwenendo wa kudhibiti mambo na kulinda mamlaka ya ardhi yote ya nchi hiyo ni kibarua kigumu. Amesisitiza kwamba, uungaji mkono wa madola ajinabi kwa makundi ya wabeba silaha kusini mwa Libya kumeikokota nchi hiyo upande wa mgogoro mkubwa zaidi.

Mufti Mkuu wa Libya, Sheikh Sadiq Al-Gharyani naye ameashiria njama za Saudi Arabia na Imarati dhidi ya Libya na  eneo zima la Mashariki ya Kati Afrika Kaskazini na kusema kuwa, pesa chafu za Imarati na Saudia zimekuwa zikitumika kuwaajiri mamluki wa Kiafrika kwa ajili ya kuikalia kwa mabavu nchi hiyo ya Kiafrika.

Katika mazingira kama haya inaonekana kuwa, viongozi wa Libya wamefahamu na kudiriki vyema vitisho vinavyoikabili nchi yao na ndio maana wanataka kuzuiwa kuendelea mwenendo wa uingiliaji wa kigeni katika masuala ya nchi hiyo kwa minajili ya kuleta utulivu wa kisiasa na kuandaa mazingira mwafaka kwa ajili ya kufanyika uchaguzi