Jeshi la Taifa la Libya ladhibiti asilimia 80 ya mji wa Derna
Msemaji wa Jeshi la Taifa la Libya amesema kuwa jeshi hilo linadhibiti asilimia 80 ya mji wa Derna.
Ahmad al Mismari amesema kuwa, vita vya Derna vimekuwa vita vya moja kwa moja na vimefikia kiwango cha kutiwa nguvuni na kukamatwa makamanda wa makundi ya kigaidi.
Msemaji wa Jeshi la Taifa la Libya ameashiria hatu y kukamatwa kwa al Asti Umar ambaye ni miongoni mwa makamanda wa makundi ya kigaidi na kusema: Baada ya kukamatwa kamanda huyo sasa Jeshi la Taifa la Libya litapata taarifa nyingi zinazohusiana na harakati za makundi ya kigaidi katika mji wa Derna.
Umar aliwahi kuwa afisa wa kikosi maalumu cha Jeshi la Libya na alikuwa akiongoza makundi ya kigaidi katika mji wa Derna.
Libya imekuwa katika machafuko makubwa ya ndani na mapigano ya makundi ya kigaidi tangu mwaka 2011 wakati vikosi vya jeshi la NATO vikisaidiwa na Marekani vilipoingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo na kupelekea kuondolewa madarakani kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi.