Basi linalotumia nishati ya jua ambalo watengezaji wake nchini Uganda wamedai ni kuwa la kwanza barani Afrika limezinduliwa rasmi
Basi linalotumia nishati ya jua ambalo watengezaji wake nchini Uganda wamedai ni kuwa la kwanza barani Afrika limezinduliwa rasmi.
Basi hilo la kielektroniki aina ya Kayoola linalomilikiwa na kampuni ya Kiira Motors limezinduliwa mjini Kampala na kutoa msisimko wa aina yake miongoni mwa wakaazi wa jiji hilo.
Mojawapo ya betri zake zinaweza kuwekwa chaji na vibamba vya umeme wa jua katika paa la nyumba ambavyo huongeza kasi ya gari hilo hadi kilomita 80 kwa saa.
Mkurugenzi mkuu wa Kiira Motors Paul Isaac Musasizi amesema kwamba amefurahishwa na mafanikio ya wahandisi wa Uganda.
Raia wamefurahishwa na wazo kwamba Uganda ina uwezo wa kutengeza mfano kama huu na Bw. Musasizi anasema kwamba angependelea kulisaidia taifa hilo kushindana na kampuni nyengine za magari katika eneo hili.
Pia anatumai kwamba hatua hiyo itabuni ajira zifikazo 7000 kufikia mwaka 2018. Lengo ni kwamba kufikia 2039, kampuni hiyo itakuwa na uwezo wa kutengeza vifaa vya magari na kuviunganisha nchini Uganda bila kutegemea kampuni nyengine.