Wahajiri haramu 191 waokolewa katika pwani za Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i46050-wahajiri_haramu_191_waokolewa_katika_pwani_za_libya
Askari wa gadi ya pwani ya Libya wamewaokoa wahajiri haramu 191 katika pwani za nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 19, 2018 03:06 UTC
  • Wahajiri haramu 191 waokolewa katika pwani za Libya

Askari wa gadi ya pwani ya Libya wamewaokoa wahajiri haramu 191 katika pwani za nchi hiyo.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa askari wa gadi ya pwani ya Libya wamewaokoa wahajiri haramu 115 katika maji ya pwani ya magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli na wengine 76 katika pwani za mji wa Az-Zawayah magharibi mwa nchi.

Hata hivyo wahajiri watano walikuwa wameshaaga dunia wakati askari wa gadi ya pwani ya Libya walipowasili kuwaokoa watu hao katika maji ya pwani ya magharibi mwa Tripoli.

Maafisa wa kikosi cha gadi ya pwani ya Libya wametangaza kuwa wahajiri haramu 115 waliookolewa, ambao ni raia kutoka nchi tofauti za Kiafrika na Kiarabu wamerejshwa mjini Tripoli.

Boti za doria za kikosi cha gadi ya pwani ya Libya

Libya ni kivuko muhimu zaidi kinachotumiwa na wahajiri wa Kiafrika katika safari zao za kuelekea barani Ulaya.

Wafanyamagendo ya binadamu wanaoitumia vibaya hali ya mchafukoge na kuvurugika amani nchini Libya husafirisha kila mwaka kwa ajili ya kuwapeleka Ulaya makumi ya maelfu ya wahajiri haramu kupitia nchi hiyo mkabala na kulipwa kitita kikubwa cha fedha na wahajiri hao. Hata hivyo idadi kubwa ya watu hao hufia njiani kabla ya kufika mwisho wa safari yao.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2018 hadi kufikia sasa, zaidi ya wahajiri haramu 7,000 wamerejeshwa nchini Libya.../