WHO yachukua hatua za kudhibiti kirusi cha Ebola Kongo DR
Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kuwa limechukua hatua za kukabiliana na kuenea kirusi cha ugonjwa wa ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
WHO imetangaza kuwa imechukua hatua ya kutuma vifaa na wafanyakazi wanaohitajika katika maeneo ya nchi hiyo yaliyokumbwa na ugonjwa wa ebola.
Wiki moja baada ya kutangazwa kudhibitiwa maambukizi ya ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, maambukizi mapya ya kirusi cha ugonjwa huo yanatishia maisha ya watu katika eneo la Beni mashariki mwa nchi hiyo.
Mripuko wa ugonjwa hatari wa ebola uliripotiwa tarehe 8 Mei mwaka huu katika mji wa Bikoro mkoani Équateur kaskazini magharibi mwa nchi na baadaye ukaenea kwenye mji wa Mbandaka katikati mwa mkoa huo.
Watu zaidi ya 11,300 walifariki dunia katika nchi kadhaa za magharibi mwa Afrika kuanzia mwaka 2013 hadi 2016 kutokana na kuugua ugonjwa huo.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Liberia, Guinea na Sierra Leone zimeathirika sana kutokana na mripuko wa ugonjwa wa ebola.../