Maelfu wakimbia makazi yao magharibi mwa Niger
(last modified Fri, 17 Aug 2018 07:50:58 GMT )
Aug 17, 2018 07:50 UTC
  • Maelfu wakimbia makazi yao magharibi mwa Niger

Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, zaidi ya watu elfu 17 wamekimbia makazi yao huko magharibi mwa Niger tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2018.

Ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa watu elfu 17, 382 wamelazimika kukimbia makazi yao magharibi mwa Niger kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na makundi ya waasi. 

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa, kuna uwezekano wa idadi ya wakimbizi hao kuongezeka iwapo hali ya usalama itazidi kuwa mbaya katika maeneo hayo. 

Maelfu wamekimbia makazi yao Niger

Ofisi ya Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa eneo la magharibi mwa Niger linalopakana na nchi ya Mali linasumbuliwa na machafuko na ukosefu wa amani kutokana na mashambulizi yanayofanywa na makundi ya waasi. Imesema kuwa eneo hilo pia linasumbuliwa na mapigano ya kikabila yanayoendelea katika eneo la Tillabéri. 

Tags