Usitishwaji mapigano watangazwa Tripoli, Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47747-usitishwaji_mapigano_watangazwa_tripoli_libya
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Libya Abdulsalam Ashour amesema kuwa makubaliano ya kusimamisha mapigano yamefikiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli, kufuatia mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo wenye silaha.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 28, 2018 14:05 UTC
  • Usitishwaji mapigano watangazwa Tripoli, Libya

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Libya Abdulsalam Ashour amesema kuwa makubaliano ya kusimamisha mapigano yamefikiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli, kufuatia mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo wenye silaha.

Ashour amesema hayo katika kituo cha televisheni nchini humo, na kuongeza kuwa makubaliano hayo yamefikiwa baada ya Idara ya Usalama ya Tripoli kudhibiti maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na wapiganaji hao.

Watu watano waliuawa na wengine 33 kujeruhiwa Jumatatu katika mapigano makali yaliyojiri mjini Tripoli. Mazungumzo zaidi yanatarajiwa kufanyika ili kufikia maptano ya kudumu ya usitishwaji vita.

Ni vyema kuashiria kuwa, Libya ina serikali mbili hasimu, moja ikiwa na makao yake mjini Tobruk na nyingine ya Umoja wa Kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli.

Libya ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa na hali ya mchafukoge tangu kupinduliwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi kufuatia uingiliaji kijeshi wa Marekani na waitifaki wake katika Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO).