LHRC: Ubakaji watoto umeongezeka Tanzania
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47832-lhrc_ubakaji_watoto_umeongezeka_tanzania
Shirika moja la haki za binadamu nchini Tanzania limesema kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la vitendo vya ubakaji nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 01, 2018 09:35 UTC
  • LHRC: Ubakaji watoto umeongezeka Tanzania

Shirika moja la haki za binadamu nchini Tanzania limesema kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la vitendo vya ubakaji nchini humo.

Ripoti ya Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) inaonyesha kuwa katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo wa mwaka 2018 watoto 2365 walibakwa, takwimu ambazo ni sawa na watoto 394 kwa siku.

Ripoti hiyo inasema katika kipinidi cha miezi sita ya kwanza kwa mwaka 2018 matukio ya ukatili kwa watoto yaliyoripotiwa ni 6376 na matukio ya 2365 yakitokana na ubakaji.

Idadi hiyo imeongezeka maradufu, ikilinganishwa na ripoti ya nusu mwaka ya mwaka jana ambayo ilionyesha watoto 759 walibakwa.

Akiwasilisha ripoti hiyo mtafiti wa Kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania, Fundikira Wazambi ameeleza kwamba vitendo hivyo mara nyingi hufanywa na ndugu wa karibu na majirani.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania, LHRC Anna Henga

Kuchapishwa kwa ripoti hiyo kunakuja wakati matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto yakiripotiwa katika nchi mbalimbali barani Afrika.

Hata hivyo, kuporomoka maadili ambako kumesababishwa na mitandao ya kijamii kunatajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochochea vitendo cha ukatili katika jamii.