Watu wenye silaha washambulia makao makuu ya Shirika la Mafuta la Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48044-watu_wenye_silaha_washambulia_makao_makuu_ya_shirika_la_mafuta_la_libya
Watu kadhaa waliokuwa na silaha leo Jumatatu wameyashambulia makao makuu ya Shirika la Taifa la Mafuta la Libya (NOC) huko Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo. Watu walioshuhudia wamesema kuwa, sauti za milipuko zilisika kabla ya watu waliojeruhiwa kutolewa katika jengo la shirika hilo kwa kutumia magari ya ambulansi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 10, 2018 10:11 UTC
  • Watu wenye silaha washambulia makao makuu ya Shirika la Mafuta la Libya

Watu kadhaa waliokuwa na silaha leo Jumatatu wameyashambulia makao makuu ya Shirika la Taifa la Mafuta la Libya (NOC) huko Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo. Watu walioshuhudia wamesema kuwa, sauti za milipuko zilisika kabla ya watu waliojeruhiwa kutolewa katika jengo la shirika hilo kwa kutumia magari ya ambulansi.

Shambulio hilo katika makao makuu ya Shirika la Taifa la Mafuta la Libya mjini Tripoli limefanywa na watu waliokuwa na silaha katika kipindi cha chini ya wiki moja baada ya kusimamishwa mapigano makali kati ya makundi hasimu kupitia makubaliano yanayolegalega kati ya pande hizo. Hadi sas a hakuna kundi lilotangaza kuhusika na shambulio hilo.

Itakumbukwa kuwa wanamgambo watiifu kwa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh mara kwa mara wamekuwa wakifanya mashambulizi mjini Tripoli na katika miji mingine ya Libya.

Libya imegawanyika katika sehemu mbili ziazodhibitiwa na pande mbili hasimu, suala linalosababisha mkwamo wa kisiasa na mgogoro wa kiuchumi nchini humo.