Kagame akasirishwa na wanaosema amewaachilia huru wafungwa kwa mashinikizo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48257-kagame_akasirishwa_na_wanaosema_amewaachilia_huru_wafungwa_kwa_mashinikizo
Rais Paul Kagame wa Rwanda ameoneshwa kukasirishwa sana na wale wanaosema kuwa amewaachilia huru wafungwa kutokana na mashinikizo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 20, 2018 01:33 UTC

Rais Paul Kagame wa Rwanda ameoneshwa kukasirishwa sana na wale wanaosema kuwa amewaachilia huru wafungwa kutokana na mashinikizo.

Vilevile Kagame amemuonya mwanasiasa wa upinzani Victoire Ingabire aliyeachiliwa huru mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba, atakabiliwa na uwezekano wa kurejeshwa gerezani endapo ataendelea na kile Kagame alichokitaja kama majigambo yake ya hapa na pale ya kwamba hakuomba msamaha wa kuchiliwa huru. 

Mwandishi wetu wa Rwanda, Sylvanus Karemera ametuandalia ripoti maalumu kuhusu habari hiyo...