Al Bashir: Eneo la Halayeb ni milki ya Sudan
(last modified Sun, 30 Sep 2018 14:08:03 GMT )
Sep 30, 2018 14:08 UTC
  • Al Bashir: Eneo la Halayeb ni milki ya Sudan

Rais wa Sudan amesema tena kwamba eneo linalogombaniwa la Halayeb ni milki ya nchi yake na kwamba Khartoum inazo nyaraka za kihistoria zinazothibitisha madai hayo.

Omar al Bashir amesema kuwa, Khartoum ina nyaraka zinazoonesha kwamba, Halayeb ni mali ya Sudan na hayo yanathibitishwa na nyaraka za kihistoria.

Al Bashir ameongeza kuwa, kadhia ya Halayeb ndiyo maudhui kuu ya mazungumzo ya viongozi wa kisiasa wa nchi yake ya Misri. 

Ameongeza kuwa pande mbili zina hamu ya kuimarisha uhusiano na kwamba Sudan inataka kufikia mapatano na Misri katika masuala yote yanayohusiana na hitilafu za mpaka, biashara na mahusiano ya mataifa ya nchi hizo mbili. 

Eneo la Halayeb limekuwa likigombaniwa na Misri na Sudan tangu baada ya Sudan kupata uhuru mwaka 1956 na Khartoum inaituhumu Cairo kuwa inalikalia kwa mabavu. Sudan pia imewasilisha mashtaka dhidi ya Misri katika Umoja wa Mataifa. 

Eneo la Halayeb katika ramani

Pamoja na hayo maafisa wa Misri na Sudan wamekubaliana kwamba, hitilafu juu ya umiliki wa eneo la Halayeb zisiwe sababu ya mizozo na mivutano katika uhusiano wa nchi hizo mbili. 

Tags