Umoja wa Ulaya watajwa kushiriki katika mauaji ya raia nchini Mali
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48503-umoja_wa_ulaya_watajwa_kushiriki_katika_mauaji_ya_raia_nchini_mali
Gazeti la kila wili la Der Spiegel la nchini Ujerumani limeandika habari ya uungaji mkono wa kifedha wa Umoja wa Ulaya katika mauaji ya raia na ukiukaji wa haki za binaadamu nchini Mali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 01, 2018 04:38 UTC
  • Umoja wa Ulaya watajwa kushiriki katika mauaji ya raia nchini Mali

Gazeti la kila wili la Der Spiegel la nchini Ujerumani limeandika habari ya uungaji mkono wa kifedha wa Umoja wa Ulaya katika mauaji ya raia na ukiukaji wa haki za binaadamu nchini Mali.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, EU imeupatia kiasi cha Euro milioni 100 muungano wa nchi tano ambao ulitakiwa kuwa na nafasi ya kupunguza kiwango cha wahajiri wanaoelekea nchi za umoja huo. Limezidi kufafanua kuwa, askari wa muungano wa nchi hizo wamehusika katika kukiuka haki za binaadamu yakiwemo pia mauaji ya raia. 

Raia wa Mali

Der Spiegel limeandika kuwa, kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi wa wataalamu wa operesheni za askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, katika kipindi cha mwezi Machi, Aprili na Mei mwaka huu, askari wa nchi hiyo waliteketeza makazi ya raia sambamba na kuwapiga risasi wananchi. Suala hilo limeisababishia changamoto nzito kamisheni ya Umoja wa Ulaya kwa kuwa, kwa mujibu wa sheria za umoja huo, wakati wowote EU inapowaunga mkono askari wa usalama wa nchi ya tatu, huwa inatakiwa kusimamia suala la haki za binaadamu ndani ya nchi hiyo.