Zaidi ya watu elfu 70 wakimbia machafuko ya kikabila magharibi mwa Ethiopia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48538-zaidi_ya_watu_elfu_70_wakimbia_machafuko_ya_kikabila_magharibi_mwa_ethiopia
Zaidi ya watu elfu 70 wamekimbia machafuko na ghasia za kikabila huko magharibi mwa Ethiopia. Machafuko hayo yanatajwa kuwa ni sehemu ya ghasia zilizoikumba Ethiopia katika siku za hivi karibuni na kuzidisha mashinikizo kwa serikali ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Oct 02, 2018 12:35 UTC
  • Zaidi ya watu elfu 70 wakimbia machafuko ya kikabila magharibi mwa Ethiopia

Zaidi ya watu elfu 70 wamekimbia machafuko na ghasia za kikabila huko magharibi mwa Ethiopia. Machafuko hayo yanatajwa kuwa ni sehemu ya ghasia zilizoikumba Ethiopia katika siku za hivi karibuni na kuzidisha mashinikizo kwa serikali ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed.

Wakazi wa eneo la Benishangul-Gumuz wanasema kuwa, machafuko hayo yaliripuka siku ya Ijumaa iliyopita baada ya maafisa wa wanne wa serikali za mitaa kuuawa wakati walipokuwa ziarani katika jimbo la Oromiya.

Baada ya mauaji hayo watu wa kabila la Oromo wanaoishi eneo la Benishangul-Gumuz walishambuliwa na makabila mengine na wengi wao wamekimbilia katika eneo la Oromiya.

Mamlaka ya eneo hilo imetangaza leo kuwa, idadi ya watu waliokimbia nyumba na makazi yao imepita elfu 70.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.

Machafuko hayo yamezidisha mashinikizo kwa serikali ya Waziri Mkuu wa sasa wa Ethiopia, Abiy Ahmed ambaye alishika madaraka mwezi Aprili mwaka huu na kuzusha mtikisiko wa kisiasa kwa kufanya suluhu na hasimu wa siku nyingi wa nchi hiyo, Eritrea, kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa na kuahidi kufanya mageuzi makubwa ya kisiasa na kiuchumi.   

Vilevile ameahidi kukomesha machafujo ya kikabila na kusitisha siasa kali za masuala ya usalama zilizotawala Ethiopia kwa miongo kadhaa.