Kwa mara ya kwanza, Mwislamu mwanamke ateuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi Ethiopia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48858-kwa_mara_ya_kwanza_mwislamu_mwanamke_ateuliwa_kuwa_waziri_wa_ulinzi_ethiopia
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali amemteua mwanamke Mwislamu kuwa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, hii ikiwa ni mara ya kwanza kabisa katika historia ya nchi hiyo.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Oct 17, 2018 05:25 UTC
  • Kwa mara ya kwanza, Mwislamu mwanamke ateuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi Ethiopia

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali amemteua mwanamke Mwislamu kuwa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, hii ikiwa ni mara ya kwanza kabisa katika historia ya nchi hiyo.

Abiy Ahmed Ali amemteua mwanamke Mwislamu Aisha Mohammed kuwa Waziri  mpya wa Ulinzi wa Ethiopia. 

Waziri Mkuu wa Ethiopa amebadilisha mawaziri 16 katika serikali ya nchi hiyo na kupunguza idadi ya wizara ya serikali kutoka 28 hadi 20. Nusu ya mawaziri wapya wa baraza la mawaziri la Ethiopia inaundwa na wanawake.

Chama tawala nchini Ethiopia kilimchagua Abiy Ahmed Ali kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo baada ya kujiengua waziri mkuu wa zamani, Hailemariam Desalegn ambaye kipindi cha uongozi wake kiliandamana na ukandamizaji mkubwa wa wapinzani wa serikali. 

Awali Bunge la Ethiopia lilikuwa limechukua hatua ya aina yake nchini humo na kumteua mwanamke Muislamu, Muferiat Kamil kuwa spika wa bunge hilo. Hata hivyo Bi Muferiat Kamil alijiuzulu nafasi hiyo siku chache zilizopita na kuteuliwa kama Waziri wa Amani.