Sheikh wa Azhar alaani mauaji ya kigaidi dhidi ya Wakristo nchini Misri
(last modified Sat, 03 Nov 2018 14:28:52 GMT )
Nov 03, 2018 14:28 UTC
  • Sheikh Ahmed el-Tayeb
    Sheikh Ahmed el-Tayeb

Sheikh Mkuu wa al Azhar amelaani shambulizi la kigaidi lililolenga Wakristo wa Kikopti nchini humo.

Sheikh Ahmed el-Tayeb amefanya mazungumzo ya simu na Papa Tawadros II, Kiongozi wa Wakristo wa Kikopti nchini Misri na kulaani shambulizi la kigaidi lililolenga basi la Wakopti katika mkoa wa Sohag na ametoa salamu za rambirambi na mkono wa pole kwa Wakristo nchini humo.

Sheikh wa al Azhar amelaani mashambulizi yanayowalenga Wakristo nchini Misri na kusema: Kuwashambulia Wakristo ni sawa na kulishambulia taifa zima la Misri, Waislamu kwa Wakristo.

Shambulizi la kigaidi lililolenga basi la Wakristo wa Kikopti katika mkoa wa Sohag nchini Misri limeua watu saba na kujeruhi wengine 14.

Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuwa ndilo lililofanya shambulizi hilo.    

Tags