Idadi ya waliofariki katika ajali ya boti Uganda yafika 35
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i49766-idadi_ya_waliofariki_katika_ajali_ya_boti_uganda_yafika_35
Naibu msemaji wa jeshi la Uganda Luteni kanali Deo Akiiki amesema idadi ya vifo vilivyotokana na ajali ya kupinduka kwa boti iliyotokea Jumamosi kwenye Ziwa Victoria nchini humo, imefikia 35.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Nov 26, 2018 04:33 UTC
  • Idadi ya waliofariki katika ajali ya boti Uganda yafika 35

Naibu msemaji wa jeshi la Uganda Luteni kanali Deo Akiiki amesema idadi ya vifo vilivyotokana na ajali ya kupinduka kwa boti iliyotokea Jumamosi kwenye Ziwa Victoria nchini humo, imefikia 35.

Msemaji huyo ameongeza kuwa operesheni za uokoaji na utafutaji wa miili, zitaendelea kwa wiki moja au zaidi lakini kuna uwekezano mdogo wa kuwapata walionusurika.

Imeelezwa kuwa boti hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 50, ilibeba watu 150 jambo lililopelekea kuzama muda mfupi baada ya kuanza safari mjini Mpatta wilayani Mukono.

Taarifa zinasema Prince David Wasajja, ndugu wa mfalme wa Buganda Mfalme Kabaka Ronald Mutebi alikuwa pia kwenye mashua hiyo lakini aliokolewa,

Rais Museveni wa Uganda

Kufuatia ajali hiyo, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametuma salamu za rambi rambi na kumtaka nahodha wa boti hiyo achukuliwe hatua za kisheria.

Miezi miwili iliyopita, watu zaidi ya 200 walipoteza maisha katika nchi jirani ya Tanzania baada ya kuzama kwa Ferry katika ziwa hilo ambalo linamilikiwa na nchi za Afrika Mashariki ya Kenya, Uganda na Tanzania.