Waziri Mkuu wa Ethiopia akutana na wapinzani, aahidi uchaguzi huru, wa haki
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i49797-waziri_mkuu_wa_ethiopia_akutana_na_wapinzani_aahidi_uchaguzi_huru_wa_haki
Waziri Mkuu wa Ethiopia amekutana na wajumbe wa vyama 81 vya siasa kujadili njia za marekebisho ya mfumo wa uchaguzi wa nchi hiyo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Nov 27, 2018 11:21 UTC
  • Waziri Mkuu wa Ethiopia akutana na wapinzani, aahidi uchaguzi huru, wa haki

Waziri Mkuu wa Ethiopia amekutana na wajumbe wa vyama 81 vya siasa kujadili njia za marekebisho ya mfumo wa uchaguzi wa nchi hiyo.

Hatua hiyo ya Abi Ahmed ni sehemu ya jitihada za kutekeleza ahadi yake ya kuanzisha anga huru ya kisiasa nchini Ethiopia baada ya kudhibitiwa na chama tawala kwa miaka mingi.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia imesema kuwa, mkutano huo ulijadili marekebisho yanayotakiwa ili kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa huru na wa haki na kushirikishwa makundi na vyama vyote katika mchakato huo.

Tangu alipochukua madaraka ya nchi mwezi Aprili mwaka huu, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amechukua hatua muhimu za marekebisho ya kisiasa ikwa ni pamoja na kuwaruhusu wapinzani waliokuwa nje ya nchi kurejea nyumbani, kuwaachia huru maelfu ya wafungwa wa kisiasa na kumteua mpinzani wa zamani aliyewahi kufungwa jela kuwa Mkuu wa Tume ya Uchaguzi.

Birtukan Mideksa ameteuliwa kwua Mkuu wa Tume ya Uchaguzi, Ethiopia.

Vilevile amewateua wanawake 10 kuwa mawaziri na kuifanya nchi hiyo iwe ya tatu baada ya Rwanda na Ushelisheli, kuwa na baraza la mawaziri lenye asilimia 50 ya mawaziri wanawake barani Afrika.

Katika mkondo huo huo Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali amemteua mwanamke Mwislamu kuwa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, hii ikiwa ni mara ya kwanza kabisa katika historia ya nchi hiyo.