NIgeria: Upo udharura wa kuzidishwa mawasiliano na ushirikiano ili kupambana na ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i5002-nigeria_upo_udharura_wa_kuzidishwa_mawasiliano_na_ushirikiano_ili_kupambana_na_ugaidi
Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria imesisitiza juu ya ulazima wa kuzidishwa mawasiliano na ushirikiano unaohitajika kati ya nchi za eneo ili kupambana na kundi la Boko Haram.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 14, 2016 03:53 UTC
  • NIgeria: Upo udharura wa kuzidishwa mawasiliano na ushirikiano ili kupambana na ugaidi

Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria imesisitiza juu ya ulazima wa kuzidishwa mawasiliano na ushirikiano unaohitajika kati ya nchi za eneo ili kupambana na kundi la Boko Haram.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria iimetangaza kuwa kundi la Boko Haram katika kipindi cha miezi iliyopita limepata pigo kali kutoka vikosi vya majeshi ya nchi za eneo, hata hivyo kwa bahati mbaya kundi hilo lingali linaendeleza hujuma zake za kigaidi.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria imeongeza kuwa, maafisa usalama wa Nigeia, Chad na Niger hadi sasa wameshindwa kuratibu oparesheni za majeshi ya nchi hizo dhidi ya Boko Haram katika eneo na hivyo kundi hilo kutumia vibaya nukta hiyo ya udhaifu.

Maafisa usalama wa nchi hizo tatu mwaka jana walikutana Abuja kwa lengo la kutathmini oparesheni zao za pamoja dhidi ya kundi la Boko Haram.

Hadi kufikia sasa, watu zaidi ya milioni mbili wameyahama makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani tangu kuanza mapigano na mashambulizi ya Boko Haram huko Nigeria.