Ethiopia yawakamata waliohusika na mauaji ya mafisa wa serikali
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50412-ethiopia_yawakamata_waliohusika_na_mauaji_ya_mafisa_wa_serikali
Ethiopia imewakamata watu 15 wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya viongozi wa serikali za mitaa. Taarifa iliyotolewa na idara ya mawasiliano ya jimbo la Oromia inasema watu hao 15 wanashukiwa kuwaua maofisa wa serikali wa jimbo hili, na kuwalenga maofisa wa usalama.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 25, 2018 04:36 UTC
  • Ethiopia yawakamata waliohusika na mauaji ya mafisa wa serikali

Ethiopia imewakamata watu 15 wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya viongozi wa serikali za mitaa. Taarifa iliyotolewa na idara ya mawasiliano ya jimbo la Oromia inasema watu hao 15 wanashukiwa kuwaua maofisa wa serikali wa jimbo hili, na kuwalenga maofisa wa usalama.

Idara hiyo pia imesema bunduki kadhaa, maguruneti na silaha nyingine pia zimekamatwa pamoja na watuhumiwa hao. Watu hao wanadhaniwa kuwa na uhusiano na makundi yenye silaha, hasa kundi la Harakati ya Ukombozi ya Oromo (OLF).

Kundi la Harakati ya Ukombozi ya Oromo linakadiriwa kuwa na wapiganaji 2,800 wakiwa sehemu ya magharibi ya jimbo la Oromia, katika miezi ya hivi karibuni limekuwa likifanya mashambulizi dhidi ya jeshi na raia.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Aby Ahmed

Wiki hii pia watu 7 waliuawa katika mapigano ya kikabila yaliyotokea katika jimbo la Amhara, kaskazini mwa Ethiopia.

Hivi karibuni pia watu 23 waliuawa katika machafuko yaliyozuka jirani na mji mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa, baada ya wafuasi wa kundi la zamani la waasi la Harakati ya Ukombozi wa Oromo (OLF) ambao wengi wao wanatoka katika kabila la Oromo, kuingia mjini Addis Ababa wakipeperusha bendera ya OLF na kupambana na wakazi wa mji huo.