Libya yamkosoa Mjumbe wa Umoja wa Mataifa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i5050-libya_yamkosoa_mjumbe_wa_umoja_wa_mataifa
Spika wa bunge la Libya amemkosoa Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya nchi hiyo kutokana na kuanza kazi serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo bila ya bunge kuipigia kura ya kuwa na imani nayo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 14, 2016 10:05 UTC
  • Libya yamkosoa Mjumbe wa Umoja wa Mataifa

Spika wa bunge la Libya amemkosoa Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya nchi hiyo kutokana na kuanza kazi serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo bila ya bunge kuipigia kura ya kuwa na imani nayo.

Aguillah Saleh Spika wa bunge la Libya amesema kuwa Martin Kobler Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya ameandaa mazingira ya kuanza kuasisiwa serikali ya umoja wa kitaifa na kuanza kazi serikali hiyo huko Tripoli, kabla ya bunge kuipigia kura ya kuwa na imani nayo.

Aguillah Saleh Issa ameongeza kuwa, hatua ya serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya ya kuanza kazi na kuhamia Tripoli ni kinyume na makubaliano ya Sakhirat yaliyosainiwa kati ya pande za Libya chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.

Bunge la Libya linataraji kuipigia kura ya kuwa na imani serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo tarehe 18 mwezi huu.

Nazo nchi za Magharibi zinataraji kuwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al Siraj itaweza kulinda umoja wa kitaifa wa nchi hiyo na kuendesha vita dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh kwa kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa.