Polisi Kenya yazima shambulio jingine la al Shabaab
(last modified Mon, 21 Jan 2019 16:34:39 GMT )
Jan 21, 2019 16:34 UTC
  • Polisi Kenya yazima shambulio jingine la al Shabaab

Polisi ya Kenya imezima shambulio la wanamgambo wanaoshukiwa kuwa ni wa kundi la kigaidi la al Shabaab katika kampuni moja ya ujenzi inayomilikiwa na Wachina magharibi mwa nchi hiyo. Hayo yamesemwa leo na afisa mmoja wa Kenya siku chache baada ya kundi hilo la kigaidi kuuwa watu 21 jijini Nairobi.

Wavamizi hao wamemjeruhi mtu mmoja wakati wakijaribu kuvamia eneo hilo la kampuni hiyo ya ujenzi inayomilikiwa na Wachina katika barabara ya kuu ya Garissa-Modogashe; eneo ambalo si mbali kutoka katika mpaka wa Kenya na Somalia. David Kerina, Kamanda wa Polisi wa Kaunti  ya Garissa ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa wavamizi hao walijibiwa haraka kwani maafisa usalama wako katika hali ya tahadhari. Magaidi wanne wameuawa katika shambulio hilo.

Shambulio la karibuni la wanamgambo wa al Shabaab jijini Nairobi

Kamanda Kerina ameongeza kuwa, milio ya risasi ilisikika kabla ya wavamizi kukimbia na kwamba mtu aliyejeruhiwa alikuwa ni mke wa mlinzi wa kampuni hiyo.

Kamanda huyo wa polisi ya kaunti ya Garissa amesema kuwa, anaamini kwamba wavamizi hao ambao walikuwa na silaha huenda ni wanamgambo wa al Shabaab. Amesema kwa sasa wamezidisha operesheni za kiusalama nchini Kenya na kwamba bado hawajamtia mbaroni mtu yoyote kuhusiana na shambulio hilo la huko Garissa.

Tags