Libya yaanza ujenzi wa ukuta katika mpaka wa pamoja na Misri
(last modified Tue, 22 Jan 2019 14:59:41 GMT )
Jan 22, 2019 14:59 UTC
  • Libya yaanza ujenzi wa ukuta katika mpaka wa pamoja na Misri

Serikali ya Libya imeanzisha ujenzi wa ukuta katika mpaka wa pamoja na Misri kwa lengo la kuzuia kuingia wanachama wa kigaidi katika nchi hiyo.

Milud Jawad, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya mashariki mwa Libya yenye mafungamano na Kamanda Khalifa Belqasim Haftar katika mji wa Tobruk, amesema kwamba wizara hiyo imeanza kazi ya ujenzi wa ukuta huo katika mpakana wa pamoja na Misri na katika viunga vya kivuko cha mpaka wa Musaid. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ukuta huo wenye mwinuko wa mita tatu, utakuwa pia moja ya vizuizi ambavyo vitazuia kupenya wahamiaji haramu kutoka Misri kwenda Libya. Viongozi wa Misri na katika kuzuia upenyaji wa magaidi kutoka Libya kuingia nchi hiyo wametangaza kuchukua uamuzi wa kufunga kivuko cha Sallum katika mpakana wa pmoja na Libya sambamba na kuzuia kuingia magairi ya mizigo kutoka Libya.

Wahajiri wanaotumia mipaka ya Misri na Libya

Jumatatu ya jana pia viongozi wa Misri walizuia kuingia nchini humo raia kadhaa wa Libya na kuwalazimisha kuchukua vibali vya kuingia nchi hiyo. Katika miaka ya hivi karibuni Misri inakabiliwa na ongezeko la wahajiri haramu. Akthari ya wafanya magendo ya binaadamu wanatumia ardhi ya Libya kwa ajili ya kuwavusha wahajiri hao kupitia bahari ya Mediterranean kwenda barani Ulaya.

Tags