Foreign Policy: Waziri Mkuu wa Ethiopia ni mwanafikra wa kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i51127-foreign_policy_waziri_mkuu_wa_ethiopia_ni_mwanafikra_wa_kimataifa
Jarida la Foreign Policy limemtaja Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia kuwa mwanafikra wa kimataifa kutokana na jitihada zake za kitaifa na kieneo ndani ya miezi 12 iliyopita.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jan 26, 2019 04:44 UTC
  • Foreign Policy: Waziri Mkuu wa Ethiopia ni mwanafikra wa kimataifa

Jarida la Foreign Policy limemtaja Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia kuwa mwanafikra wa kimataifa kutokana na jitihada zake za kitaifa na kieneo ndani ya miezi 12 iliyopita.

Jarida hilo limesema ndani ya miezi tisa katika uongozi wake, Abiy amefanya mabadiliko mengi katika nyuga za uchumi, siasa na diplomasia mbali na kuhuisha uhusiano na majirani zake.

Serikali ya Abiy Ahmed imewaachia huru maelfu ya wafungwa wa kisiasa katika fremu ya marekebisho ya haraka ya kisiasa na kiuchumi ambayo yanashuhudiwa katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika  tokea Waziri Mkuu, Abiy Ahmed aingie madarakani mwezi Aprili mwaka jana. 

Abiy (kushoto) akiwa na Rais wa Eritrea

Mbali na jitihada zake ndani ya nchi, Abiy pia amekuwa mbioni kufufua uhusiano wa nchi hiyo na nchi za kieneo. Julai 9 mwaka jana, Waziri Mkuu huyo wa Ethiopia, na Rais wa Eritrea, Isaias Afwerki walisaini makubaliano ya kukomesha uhasama na kuhuisha uhusiano wao wa kidiplomasia katika hafla iliyofanyika mjini Asmara.