Nchi tatu za Afrika zataka Russia iwepo kijeshi katika ardhi zao
Libya, Sudan na Misri, nchi tatu za Kiarabu za bara la Afrika zimetangaza utayari wa kuwapokea askari wa Russia au kuiruhusu nchi hiyo ianzishe kituo cha kijeshi katika ardhi zao.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Sputnik, Khalifa Haftar, kamanda wa vikosi vinavyojiita jeshi la taifa la Libya amependekeza kwa Russia ikajenge kituo cha kijeshi katika mji wa pili kwa ukubwa wa nchi hiyo wa Benghazi ili kuiwezesha Moscow kuwa na sauti ya juu kijeshi kusini mwa Bahari ya Mediterania na jirani nchi wanachama wa shirika la kijeshi la NATO.
Sudan, ni nchi nyingine ya Kiarabu ambayo itaipatia Russia moja ya miji yake ya bandari ili ijenge kituo chake cha kijeshi.
Kamati ya ulinzi na usalama ya Bunge la Sudan imeashiria kukubali Russia wazo la kuingia na kutia nanga meli za kijeshi za nchi mbili katika bandari za kila upande na kutangaza kuwa hatua hiyo inaweza kuwa utangulizi wa kuanzishwa kituo cha kijeshi cha Russia nchini Sudan na katika pwani ya Bahari ya Nyekundu.
Na hii ni katika hali ambayo, kwa ridhaa ya serikali ya Sudan, hivi sasa kuna washauri wa kijeshi wa Russia nchini humo.
Shirika la habari la Sputnik, limeashiria pia hamu ya Misri ya kuwa na ushirkiano wa kijeshi na Russia na kufafanua kwamba, Cairo imeeleza kuwa iko tayari kuruhusu miundomsingi yake itumiwe na ndege za kijeshi za Russia.../