Viongozi wa Afrika wakamilisha mkutano wao Addis Ababa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i51500-viongozi_wa_afrika_wakamilisha_mkutano_wao_addis_ababa
Mkutano wa 32 viongozi wa nchi za Afrika ulimaliza kazi zake alasiri ya jana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 12, 2019 04:27 UTC
  • Viongozi wa Afrika wakamilisha mkutano wao Addis Ababa

Mkutano wa 32 viongozi wa nchi za Afrika ulimaliza kazi zake alasiri ya jana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Taarifa ya mwisho ya mkutano huo iliyosomwa na Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri imesisitiza uungaji mkono wa viongozi wa nchi za Afrika kwa suala la kuunganishwa nchi za bara hilo, kuharakisha uanzishwaji wa maeneo huru ya kibiashara, udharura wa kukarabatiwa na kujengwa upya maeneo yaliyoathiriwa na vita na kutayarisha mazingira mazuri ya kurejea wakimbizi katika makazi na maeneo yao.

Abdel Fattah al Sisi

Viongozi wa nchi za Afrika pia wametilia mkazo suala la kudumishwa jitihada za kuufanyia marekebisho Umoja wa Afrika kwa shabaha ya kuuwezesha kutimiza malengo yake, kuimarisha misingi ya ustawi na maendeleo endelevu na kutatua matatizo ya bara la Afrika.

Mkutano huo wa Umoja wa Afrika ulianza kazi zake Jumapili iliyopita mjini Addis Ababa ukiwa na ajenda ya kujadili ustawi, usalama na amani, suala la kuanzishwa maeneo huru ya biashara barani Afrika na kuimarishwa ushirikiano na taasisi za kimataifa.