Jenerali Haftar afikia mapatano na serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i51855-jenerali_haftar_afikia_mapatano_na_serikali_ya_umoja_wa_kitaifa_ya_libya
Ujumbe wa wawakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya Libya umetangaza kuwa, Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya na kamanda wa Jeshi la Taifa la nchi hiyo wamefikia makubaliano juu ya kuitisha uchaguzi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 28, 2019 12:19 UTC
  • Jenerali Haftar afikia mapatano na serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya

Ujumbe wa wawakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya Libya umetangaza kuwa, Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya na kamanda wa Jeshi la Taifa la nchi hiyo wamefikia makubaliano juu ya kuitisha uchaguzi.

Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umesema kuwa Jenerali Khalifa Haftar kamanda wa Jeshi la Taifa la Libya na Fayez  al Sarraj, Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya nchi hiyo wamefikia mapatano kuhusu namna ya kuitisha uchaguzi nchini humo.  

Khalifa Haftar na Fayez al Sarraj jana Jumatano walifanya mazungumzo ili kufikia mwafaka wa pande zote kuhusu jinsi ya kurejesha amani na utulivu huko Libya katika kikao kilichofanyika Abu Dhabi mji mkuu wa Imarati ambacho pia kilihudhuriwa na wawakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa. Baada ya mazungumzo hayo pande mbili zilikubaliano juu ya udharura wa kufanyika uchaguzi na kuunga mkono jitihada za kurejesha amani na utulivu nchini Libya. Libya imekuwa na serikali mbili na mabunge mawili  kwa wakati mmoja tangu mwaka 2014. 

Fayez al Sarraj, Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya 
 

Kuwepo serikali mbili ni miongoni mwa sababu kuu za kujiri na kuendelea hali ya mchafuko na mgogoro wa kisiasa huko Libya.