Serikali ya Tobruk, Libya yatoa hukumu ya kuachiwa huru wapambe wa Gaddafi
Serikali ya Libya yenye makao yake makuu katika mji wa Tobruk imetoa amri ya kuachiwa huru baadhi ya wanasiasa mashuhuri wa serikali ya dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Kanali Mumammar Gaddafi.
Waziri wa Sheria wa serikali ya muda wa Tobruk, Mahmoud al Fitouri ameamuru kuachiwa huru Baghdadi Ali Mahmudi aliyekuwa waziri mkuu wa mwisho wa serikali ya Muammar Gaddafi na vilevile Abdullah al Senussi ambaye alikuwa mkuu wa shirika la ujasusi la Libya katika serikali ya mwisho ya Gaddafi.
Al Fitouri amesema kuwa, wapambe hao wa Gaddafi wameachiwa huru kutokana na hali zao mbaya za kiafya.
Mwaka 2015 wapambe hao wawili wa dikteta wa zamani wa Libya pamoja na mtoto wa kiume wa Gaddafi, Seiful Islam Gaddaf, walihukuma kifo na Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa yenye makao yake makuu katika mji wa Tripoli.
Libya ilitumbukia katika machafuko na vita vya ndani baada ya wanajeshi wa Marekani wakishirikiana na wale wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) kuishambulia nchi hiyo na kusaidia harakati za kumuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi hapo mwaka 2011.
Nchi hi hiyo ina serikali na mabunge mawili tofauti.